Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezitaka bodi za mikopo ya elimu ya juu kutoa maelezo ya kina kuhusu wanafunzi 168 wa chuo kikuu cha Dar es salaam na 919 wa chuo kikuu cha Dododma  wanaoonekana kukopeshwa kiasi cha bilioni tatu ambao hawatambuliki na vyuo hivyo.

Akizungumza  na wanahabari leo jijini Dar es salaam Prof. Ndalichako amesema kuwa fedha hizo zimetumika kulipa wanafunzi hewa hivo  bodi za mikopo zinapaswa kuhakikisha zinapitia dosari zote ambazo zimejitokeza na kuwachukulia hatua mara moja wahusika wote.

Aidha ameongeza kwamba bodi hizo zinatakiwa kukamilisha mikakati hiyo ndani ya wiki mbili ikiwa ni pamoja na kupeleka ripoti za utambuzi za wanafunzi hao au kurejesha fedha hizo  kwa kuwa ni mali ya serikali.

Pamoja na hayo Waziri Ndalichako ameitaka bodi kutofanya uzembe juu ya ufuatiliaji wa ukaguzi wa wanafunzi 2619 waliotumia zaidi ya bilioni 700 za mikopo katika vyuo tofauti lakini wanatumia namba moja ya kidato cha nne.

Hata hivyo amezitaka bodi zote zilizopo ndani ya wizara yake kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa ufanisi na kujifanyia ukaguzi wenyewe pasipo kusubiri kukaguliwa na yeye ikiwa ni pamoja na bodi kusimamia taasisi zake vizuri.

Fastjet kutoa misaada kwa watoto yatima siku ya mtoto wa Afrika
Video: Aliyoyasema Kamanda Sirro kuhusu Kiongozi wa ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe