Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa muda wa wiki moja kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Ndalichako kuhakikisha anakutana na wakuu wa vyuo vikuu nchini, ili kubaini vyuo ambavyo vimeshindwa kuwasilisha mchango wa wanafunzi katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Ametoa agizo wakati akifungua mkutano mkuu wa kwanza kwa mwaka 2019/2020 wa Jumuiya ya wanafunzi ya Taasisi ya elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Mjaliwa ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi hao yaliyowasilishwa na mwenyekiti wa TAHLISO, Peter Noboye.

Noboye amesema kumekuwa na ucheleweshwaji wa vitambulisho vya Bima ya afya unaotokana na baadhi ya vyuo kuchelewesha kufikisha fedha NHIF.

Aidha, ameziagiza menejimeti zote za vyuo vikuu nchini kuendelea kushirikiana kwa ukaribu na serikali za wanafunzi kwenye vyuo vyao ili waweze kushughulikia changamoto za wanafunzi kwa wakati.

DC mpya Ilala afunguka
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 10, 2020