Vyombo vya Habari nchini vimeshauliwa kushirikiana na Baraza la Habari Kiswahili la Taifa ili kuweza kujua lugha sahihi ya kiswahili wakati wanapofikisha ujumbe kwa jamii na kueweza kuondoa mkanganyiko.

Ushauri huo umetolewa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel wakati wa ziara katika Kampuni ya  Magazeti ya Mwananchi (MCL) ambapo amesema kuwa Baraza la Kiswahili lipo kwa ajili ya kukuza  na kuendeleza Lugha ya Kiswahili hivyo vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika matumizi sahihi ya Kiswahili.

“Vyombo vya habari mna nguvu kubwa kwa jamii na mnafuatiliwa na watu wengi hivyo mnapaswa kujua matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili katika uandishi, utangazaji pamoja na matumizi mengine katika kuwasiliana na hadhira yenu,”amesema Prof. Elisante.

Amesema kuwa ni wajibu kwa wadau wa habari kusoma vizuri na kuelewa Sheria ya Huduma za Habari kwa kutambua mambo muhimu yaliyoanishwa katika Sheria hiyo ikiwemo Mikataba, Bima ya Afya, Bodi na Mfuko wa Habari utakaowawezesha kupata ufadhili wa kusoma.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Francis Nanai amesema kuwa Kampuni yake itaendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza majukumu yake kwa manufaa ya nchi.

Odinga ashindwa kutangaza msimamo wa NASA
Klabu Za Ligi Daraja Kwanza Kukutana