Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Prof. Anna Tibaijuka amesema kuwa wapo watu ndani ya Serikali ya awamu ya tano hawamuogopi Mungu ndiyo maana wanakuwa wanawaonea wananchi na kuichafua serikali pamoja na Rais Magufuli.

Ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara baada ya kuona watu wakilipishwa kodi na kupewa risiti za mwaka 2015 fedha ambazo zinaonekana hazifiki serikalini.

“Serikali ya Rais Magufuli haiwezi kukubali haya mambo wanataka tu kuchafua jina la Rais amini usiamini serikali zinahujuma ndani yake sasa watu wanatokaje Mwanza na kumlazimisha huyu mvuvi mkubwa ambaye ana mitumbwi 28, anakuja mtu mla rushwa, serikali ya Magufuli haiwezi kumtoa mtu kule aje kula rushwa huku, Rais Magufuli huyu anayelia usiku na mchana mambo yakae vizuri ila leo nitamtumia risiti zile za watu wake wamekusanya kodi hapa kwa risiti za mwaka 2015,”amesema Prof. Tibaijuka

Hata hivyo, Tibaijuka amesema kuwa yeye anaamini kuwa Rais Dkt. Magufuli hawezi kutuma watu kwenda kuchoma nyavu za wavuvi.

Wazazi wafariki dunia, mtoto anusurika
Mgogoro kati ya Uingereza na Urusi wazidi kufukuta