Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu amekosoa uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu alioufanywa hivi karibuni na rais John Magufuli.

Profesa Baregu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amesema kuwa anaushangaa uteuzi huo kwani unakinzana na dhana yake ya kutaka kupunguza ukubwa wa serikali yake.

“Tulitarajia kuwa rais Magufuli angechagua idadi ya makatibu wakuu ambayo inaakisi baraza lake la mawaziri, lakini nimeshangaa kuona kwamba kwenye baadhi ya wizara kuna makatibu wakuu wawili au watatu,” Profesa Baregu aliliambia The Citizen.

Aliongeza kuwa hivi sasa ni vigumu kufahamu kuwa nani atakuwa mtendaji mkuu kwenye wizara ambayo wameteuliwa makatibu wakuu wawili au watatu.

Naye Mkurugenzi wa Sheria katika  Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia aliungana na kauli ya Profesa Baregu na kueleza kuwa ni vyema sasa sheria ikaweka ukomo cha idadi ya watu wanaopaswa kuteuliwa kwenye ofisi husika.

 

Hizi ni picha Tano zilizopendwa zaidi mwaka 2015
Kubenea Azungumzia Tuhuma Za Wizi Wa Mali na Jina la Nduguye, Ukanjanja