Mbunge wa Mikumi, Joseph ‘Profesa Jay’ Haule, ni miongoni mwa watu walioufunga mwaka jana kwa tukio zito akigonga hodi mwaka huu akitarajia kufunga ndoa.

Profesa Jay ambaye ni nguli wa muziki wa Hip Hop, jana alimvisha rasmi pete ya uchumba mpenzi wake wa muda mrefu anayetumia jina la Mke wa Profjize kwenye mtandao wa Instagram. Mwaka huu jina hilo litakuwa na maana zaidi.

Kupitia mtandao wa Instagram, Profesa Jay alipost picha ya tukio hilo akiwa amepiga magoti kuomba ndoa, ombi ambalo hata bila kusikia alichokisema mrembo huyo, picha inaonesha anakubali kutoka moyoni.

“Asante sana Mungu, Leo tunaufunga mwaka namna hii @mke_wa_profjize @tharealsimplex @blackchatta,” Profesa Jay aliandika.

profesa-jay

Tunawatakia kila la heri ‘njiwa hawa wapendanao’, tunaamini mwaka huu tutakula ‘ubwabwa’ tukishuhudia kiapo cha pingu za maisha.

Picha: Waziri Nchemba akutana na Mama Chid Benz, aeleza alivyoguswa
Dar24: Tunakutakia Heri ya Mwaka Mpya 2017, hii ni ahadi yetu kwako