Waziri wa Katiba na Sheria Profesa  Palamagamba Kabudi amewaagiza Watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma katika utendaji wao wa kazi wa kila siku hasa katika utoaji wa haki kwa wananchi. 

Waziri Kabudi ameyasema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Mahakama na Wadau wa Sheria katika Wilaya za Singida na Halmashauri ya Mkalama huku akisisitiza kuwa Wizara yake haitawavumilia watumishi wazembe na wapenda rushwa kwani wakiachwa bila kuwajibishwa wataipaka matope Idara ya Mahakama.

“Wizara yangu haitawavumilia watumishi wazembe na wapenda rushwa kwani wakiachwa bila kuwajibishwa wataipata matope Idara ya Mahakama ili ionekane kuwa haifanyi kazi zake vizuri kumbe hali hiyo inasababishwa na watumishi wachache,” Amesema Profesa Kabudi.

Akizungumzia kuhusiana na suala la uhaba wa Watumishi wa Mahakama Kabudi amesema Serikali itahakikisha inaondoa changamoto hiyo haraka ili wananchi waweze kupata huduma bora na ya uhakika karibu na maeneo yao.

katika hatua nyingine amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufanyika kazi kwa Watumishi wa Mahakama ikiwemo kupatia vitendea kazi ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Kumwembe: Nina mashaka na usajili wa Makambo
TFNC yaja na suluhu ulishaji wa watoto kwa njia ya mtandao (E- Learning)