Katibu Mkuu wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amejibu waraka wa pasaka uliotolewa na maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), uliotakiwa kusomwa kanisani Machi 25.

Profesa Kitila ambaye ameielekeza barua yake ya majibu hayo kwa Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Askofu Frederick Shoo, kwanza amewapongeza maaskofu hao na kisha kutoa maoni yake kinzani na ushauri.

Alisema kuwa anachofahamu, kutokana na mafundisho ya dini ya Kikristo, kazi kuu za maaskofu ni zile ambazo zilifanywa na Yesu Kristo na sio vinginevyo.

Aidha, aliwashauri maaskofu hao kuhakikisha kanisa halioneshi liko upande mmoja wa hoja zenye pande mbili katika taifa ili kuepuka mgawanyiko ndani ya kanisa hilo.

“Kwa kufanya hivyo, mtaepusha migawanyiko isiyo ya lazima ndani ya kanisa na kwa nchi kwa ujumla,” ameandika Profesa Kitila katika barua yake ya Machi 29.

“Ni hatari kwa taifa kutoa kauli zenye maumivu na mafarakano badala ya kuponya,” aliongeza.

Waraka wa maaskofu wa KKKT uliosainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo uligusia masuala ya Katiba Mpya, chumi, siasa na jamii.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 1, 2018
Joshua ampiga Parker, amnyooshea ngumi Wilder