Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amepinga uamuzi uliotolewa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi mkuu muda mfupi kabla ya kutangaza matokeo ya urais.

Akiongea jana na Azam TV nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Profesa Lipumba, Profesa Lipumba aliukosoa uamuzi wa NEC na kudai kuwa haukuwa wa haki kwani sababu zilizotajwa na mwenyekiti wa ZEC hazina mashiko kwa kuwa NEC imeendelea kueleza kuwa uchaguzi ulikuwa huru na haki na kutumia matokeo ya Zanzibar katika majumuisho ya kura za urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo inatangaza matokeo ya urais wa muungano wa Tanzania, imekuwa inatangaza matokeo ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao umefanyika kwenye uchaguzi huohuo mmoja. Na Tume haijasema kwamba uchaguzi ule ulikuwa ni mbovu,” alisema Lipumba.

Aidha, Lipumba aliitaka ZEC kubatilisha uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume hiyo kwa madia kuwa haikufuata sheria na taratibu kwa kuwa haikuwahusisha wajumbe wa tume hiyo. Alisema uamuzi uliofanywa ulikuwa uamuzi binafsi.

“Hana mamlaka ya kisheria kwa sababu amevunja sheria, kungekuwa na utaratibu mzuri angepaswa labda kutumia majaji waweze kutazama tamko hili alilolitoa lina uhalali gani. Hauwezi kuzungumza bila wajumbe wa Tume ya Uchaguzi,” alisema.

Alitoa wito kwa pande zote mbili kurudi mezani na kukubaliana kuendelea na zoezi la kujumuisha kura na kuiruhusu haki ichukue mkondo wake. Alimtaka atakayetangazwa kushindwa akubali matokeo na kujiunga na atakayetangazwa kuwa mshindi ili kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

 

 

Baadhi Ya Wajumbe wa ZEC Watofautiana Na Uamuzi wa Mwenyekiti
Mkwasa Ajitetea Kwa Ibrahim Hajib