Joseph Leonard Haule, maarufu kama Professor Jay, Mbunge wa jimbo la Mikumi ametoa maoni kuhusu agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa watumishi wa Mungu wahubiri na kutoa mawaidha hadi kwenye kumbi za starehe.

”Tunaweza kubeza kuwa haiwezekani halafu baadaye akafanikiwa, dunia imebadilika unahitaji kupata neno la Mungu mahali popote ila kwenye klabu itakuwa shughuli nzito sidhani kama linawezekana,” amesema Professor Jay alipofanya mahojiano na EATV.

“Mimi sioni kama itaenda kufanikiwa kwa sababu bahati nzuri au mbaya mkuu wetu wa Mkoa amekuwa anaongea vitu vingi sana ambavyo havitekelezeki sasa nataka nione kwa hili amaejipangaje,” ameongeza nguli huyo wa hip hop.

Professor Jay, ametoa wimbo mpya alioshirikiana na ndugu zake wawili Black Rhyno, Donkoli, Mr. Teacher na Simple X uitwao ‘Kaza’.

Katika hatua nyingine mkali huyo wa hip hop amemtunuku msanii wa kizazi kipya Maua sama, kuwa ndiye malkia wa bongo fleva kutokana na kujituma na kutoa kazi nzuri.

Ameongeza kuwa anastahili kuungwa mkono na wakongwe wa muziki  kama yeye waliopitia vitu vingi mpaka kufanya vizuri katika tasnia ya muziki.

Wamitulinga, Daddy au Mr. Red Carpet kama anavyopenda kuitwa, amesema kuwa nyimbo za hip hop zimekuwa hazitoki kupata tuzo kwa sababu  watu hawajiongezi.

 

Real Madrid watua Paris, Marcelo aachwa
David de Gea azikata ngebe Real Madrid, Juventus, PSG