Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani na beki wa Brazil Thiago Silva wa Paris St-Germain wataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu baada ya ligi ya mabingwa Ulaya kumalizika mwezi Agosti.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33 tayari anaondoka PSG akiwa na rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote akiwa ameshaingia nyavuni mara 200 wakati Thiago Silva mwenye miaka 35, ataachana na timu hiyo akiwa kama nahodha.

“Ni maamuzi magumu tumefanya kuwaacha wachezaji wawili waliotengeneza heshima kubwa ya klabu yetu, lakini hakuna namna lazima safari yetu tufikie mwisho” alisema Mkurugenzi wa michezo Leonardo.

Wote wawili hao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa Juni 30, kipindi ambacho Ligue 1 ilifutwa tangu mwezi Aprili.

PSG imekusudia kuanza mazoezi Juni 22 kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa ligi ya mabingwa Ulaya, wameshajikatia nafasi ya robo fainali baada ya kuitoa Borrusia Dortmund hatua ya 16 bora.

Sera za Nyalandu na Mchungaji Msingwa Wanavyoutaka Urais 2020
Baba mbaroni kwa kuozesha mtoto wa miaka 12, "waliokula hela za ushenga kuzitapika"