Mabingwa wa soka nchini Ufaransa, huenda wakahamishia nguvu zao kwa mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi pamoja na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki Robin van Persie.

PSG wameripotiwa kufikiria hivyo, kutokana na hitaji la mshambuliaji ambalo linawakabili kwa sasa, baada ya kuondoka kwa Zlatan Ibrahimovic ambaye mkataba wake ulifikia tamati mwishoni mwa msimu uliopita.

Mtendaji mkuu wa PSG, Olivier Letang amepewa jukumu la kufanikisha mpango huo kwa kuaminiwa ana nguvu ya ushawishi wa kumng’oa mshambuliaji huyo nchini Uturuki na kuhamishia nguvu zake za kucheza soka huko Ufaransa.

Hata hivyo kiongozi huyo atalazimika kukutana na viongozi wa klabu ya Fenerbahce pamoja na wakala wa mshambuliaji huyo, ambaye aliwahi kuitumikia klabu za Arsenal na Man Utd zote za nchini England, ikiwa ni sehemu ya kuanza mchakato wa kazi aliyokabidhiwa.

Lakini pamoja na PSG kujipanga hivyo, klabu ya Fenerbahce haijawahi kutangaza hatua zozote za kumuweka sokoni Van Parsie, hali ambayo inachukuliwa kama matihani kwa Olivier Letang.

PSG wamekua wanahaha kuiziba nafasi ya Zlatan Ibrahimovic tangu alipomaliza msimu wa 2015-16.

Sugu hatarini, adaiwa kuwatusi wabunge wa CCM
Vutankuvute: CCM kuing'oa miba ya Chadema kuhusu Magufuli kila kona