Pirikapirika za usajili wa mwishoni mwa msimu huu zimeenza kushika kasi kutokana na baadhi ya vilabu kuhusishwa na ugomvi wa kuwania wachezaji wenye hadhi kubwa duniani.

Klabu ya Man Utd mapema hii leo imetajwa kuingia katika vita kali ya kumuwania mshambuliaji kutoka nchini Brazil na FC Barcelona, Neymar da Silva Santos Júnior dhidi ya klabu tajiri nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG).

Taarifa zilizochapishwa katika gazeti la L’Equipe, la nchini Ufaransa zinadai kwamba matajiri hao wa jijini Paris wameonyesha nia ya kutaka kumuwania mshambuliaji huyo, kwa kuamini anastahili kuwepo kikosini mwao.

Tayari kiasi cha pauni million 155 zimetengwa na PSG kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye kwa sasa anafanya vyema FC Barcelona kufuatia ushirikiano mzuri uliopo kati yake na Lionel Messi pamoja na Luis Suarez (MSN).

Neymar, Lionel Messi and Luis Suarez has been devsatating in attack this season

Endapo PSG Watakamilisha dili hilo, wataweka rekodi ya kumsajili mchezaji kwa gharama kubwa duniani, ambapo kwa sasa rekodi hiyo inashikwa na klabu ya Real Madrid baada ya kumsajili mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Wales, Gareth Bale mwaka 2013 kwa ada ya uhamisho wa pauni milion 85.1 akitokea Spurs.

Man Utd nao wametajwa kuwa katika mipango ya kumsajili Neymar, lakini haijaelezwa ni kiasi gani ambacho wamekitenga kwa lengo la kukamilisha mpango huo.

Wakala wa mshambuliaji huyo ambaye pia ni nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya Brazil, Wagner Ribeiro, ameulizwa kuhusu uvumi huo na kujibu ndio kwanza anausikia katika vyombo vya habari.

Amesema anaamini mchezaji wake anafurahia maisha ya FC Barcelona na tangu aliposajiliwa Camp Nou mwaka 2013, hakuwahi kumgusia suala la kuondoka ama kukwaruzana na viongozi wa klabu hiyo.

Hata hivyo wakala huyo amedai kwamba, inapendeza kwa klabu kubwa kama PSG kuhusishwa na utaratibu wa kutaka kumsajili Neymar, kutokana na kuamini kuwa ni klabu nzuri na yenye malengo makubwa.

“Neymar ana furaha katika kikosi cha Barcelona, lakini kama itatokea anaondoka na kujiunga na PSG, itapendeza kutokana na klabu hiyo kuwa na malengo yanayotaka kufanana naye.” Amesema wakala huyo kutoka nchini Brazil

PSG wameripotiwa kuwa tayari kumlipa Naymar mshahara maradufu, zaidi ya ule anaoupokea FC Barcelona wa pauni lakini mbili na ishirini na tano elfu (225,000) kwa juma.

Matajiri hao wametenga kiasi cha pauni laki tatu (300,000) kama mshahara wa Naymar ambao atakua akipokea kwa kila juma.

PSG wameanza kupanga mikakati hiyo, kufuatia mshambuliaji wao kutoka nchini Sweden, Zlatan Ibrahimovic kutangaza kuondoka utakapofika mwishoni mwa msimu huu, kufuatia mkataba wake kufikia kikomo na ameshaeleza ataelekea nchini England kujiunga na moja ya klabu za huko.

Mtanzania ahukumiwa kifo kwenye mahakama ya Al-Shabaab
Halima Mdee amtaka Magufuli arudi kwa wananchi