Mshambulaiji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameonesha kuihofia PSG kuelekea katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaopigwa kesho katika dimba la Santiago Bernabeu nchini Hispania.

Ronaldo amekiri kwamba PSG ina wachezaji wazuri na wanaoifanya kuwa bora kwa sasa, hivyo ili timu yake ipate ushindi inahitaji kuwa kwenye ubora zaidi.

Hata hivyo, nyota huyo wa Ureno, amesema wataonesha kuwa Real Madrid ni timu imara na yenye uzoefu mkubwa, na kwamba watacheza kwa nguvu kwenye mechi zote mbili dhidi ya matajiri hao wa Ufaransa na kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Ronaldo anayasema hayo baada ya wikiendi iliyopita kufunga ‘hat-trick’ yake ya kwanza kwenye La Liga msimu huu, Real Madrid ilipoibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya  Real Sociedad kwenye dimba la Saintiago Bernabeu.

Mfumo wa utambuzi na usajili barabara nchini kuanza
Kifaru amtambia Masau Bwire

Comments

comments