Uongozi wa klabu ya Tottenham umempa nafasi meneja wa kikosi chao Mauricio Roberto Pochettino Trossero, ya kusaini mkataba mpya mbao utakuwa na mshahara maradufu kuliko ule alioanza nao wakati akitokea Southampton mwaka 2014.

Spurs wamemuwekea mezani meneja huyo kutoka nchini Argentina mkataba ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni million 5.5 kwa mwaka, ikiwa ni ushaiwshi wa kumtaka asiondoke na kujiunga na klabu nyingine mwishoni mwa msimu huu.

Man Utd wamekuwa katika taarifa za kila siku juu ya kuhitaji huduma ya Pochettino ambaye ameonyesha ujasiri mkubwa wa kukiweka pazuri kikosi cha Spurs ambacho kwa msimu huu kinawania ubingwa wa nchini England.

Mwenyekiti wa klabu ya Spurs Daniel Levy, ameripotiwa kuwa na mazungumzo ya mara kwa mara na Pochettino ikiwa ni sehemu ya kuangalia uwezekano wa kuendelea kubaki klabuni hapo.

Hata hivyo mpaka sasa Pochettino, hajazungumza lolote juu ya mkataba mpya ambao unamsubiri ausaini, na badala yake amekua akisisitiza kuangalia mafanikio ya kikosi chake na kisha mambo mengine yatafuata.

Pochettino, mwenye umri wa miaka 44, ameingia katika orodha ya mameneja wa soka barani Ulaya ambao wana ushawishi mkubwa katika soka la vijana kwa kuwapa nafasi ya kushindana na timu zenye wachezaji nguli na wenye uzoefu mkubwa.

Mbali na kuwekewa mkataba wenye donge nono la fedha kwa mwaka, pia uongozi wa Spurs umemuahidi Pochettino fungu la kutosha kwa ajili ya kufanya usajili wa wachezaji utakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Juma Mgunda Afichua Siri Ya Timu Za Tanga Kudabanga Ligi Kuu
Antonio Conte Amtolea Macho Winga Wa Inter Milan