Rais wa Urusi, Vladimir Putin amekubali mwaliko wa rais wa Sudan, Omar al-Bashir anayetafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC).

Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha habari cha taifa cha Sudan imeeleza kuwa Rais Putin ataitembelea nchi hiyo kwa lengo la kudumisha ushirikiano katika sekta ya biashara.

Putin anatarajia kutembeea vyanzo vya mafuta, gesi pamoja na migodi ya dhahabu kwa lengo la kuwekeza katika sekta hiyo.

Hivi karibuni, Bashir alimpongeza Putin kwa ushindi alioupata katika uchaguzi mkuu wa taifa hilo lenye nguvu.

ICC imetoa hati mbili za kukamatwa Bashir ambapo inazitaka nchi anazozitembelea kumkamata na kumkabidhi kwa mahakama hiyo.

Wiki hii, Bashir aliitembelea Rwanda aliposhiriki kikao cha viongozi wan chi 44 za Afrika ambao walipitisha na kusaini makubalino ya kulifanya eneo hilo kuwa eneo huru la biashara.

Maneno ya busara Machi 23, 2018
Jeshi la Polisi lafanya oparesheni kali, laibua mazito