Rais wa Urusi Vladmir Putin yuko jijini Rome kwa ziara inayojumuisha mazungumzo na kiongozi wa kanisa katoliki na serikali ya Italia ya siasa kali za kizalendo, ambayo imetoa wito wa kupunguzwa kwa vikwazo licha ya mgogoro unaoendelea kwasasa kati ya Urusi na nchi za Magharibi.

Mara tu baada ya kuwasili, Rais Putin alielekea moja kwa moja katika makao makuu ya Kanisa Katoliki ambapo alifanya mazungumzo ya faragha na Papa Francis.

Aidha, mkutano huo wa leo unakuja siku moja tu kabla ya Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki kuwakaribisha viongozi wa Kanisa Katoliki la Kigiriki nchini Ukraine.

Waanaharakati wanaopigania kujitenga mashariki mwa Ukraine wengi wao ni Kanisa la Orthodox la Urusi, wakati wale wanaopingana nao ni wa Orthodox na Wakatoliki wa Ugiriki.

Hata hivyo, Ikulu ya Rais nchini Urusi imesema kuwa Putin atajadili mahusiano ya Urusi na Umoja wa Ulaya, hali nchini Syria, Ukraine na Libya na mpango wa nyuklia wa Iran.

Siwezi kuisaida Brazil kwenye fainali- Willian
Jogoo aburuzwa mahakamani kwa kuwakera majirani