Rais wa Urusi, Vladimir Putin amekiri uwepo wa wasiwasi na maswali kuhusu usaidizi wa China kuhusu vita vya Taifa lake na Ukraine baada ya kukutana na kiongozi wa China Xi Jinping huko Uzbekistan na kusema Moscow haiungwi mkono na mshirika wake huyo mwenye nguvu Duniani.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao wawili badala ya kuonyesha umoja wa Eurasia dhidi ya Magharibi, walitoa maoni tofauti kupitia hotuba zao kwa umma ambapo Puttin amesema, “Tunathamini sana msimamo wa uwiano wa marafiki zetu wa China kuhusiana na mgogoro wa Ukraine,” huku Xi akiwa hajaitaja kabisa Ukraine.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, kushoto na Kiongozi wa China, Xi Jinping, wakiwa katika mkutano wao. Picha na Alexandr Demyanchuk.

Takriban miezi saba baada ya uvamizi wake kuanza, Putin anajikuta katika hali ya kutisha ya kisiasa, ambapo tayari Urusi imepoteza zaidi ya kilomita za mraba 1,000 za eneo nchini Ukraine mwezi huu na anakabiliwa na ukosoaji usio wa kawaida kutoka kwa baadhi ya wafuasi juu ya vita.

Hata hivyo, Uchina ilisema, “itupo tayari kufanya kazi na Urusi ili kuonyesha jukumu la nchi kubwa, kuchukua jukumu kuu, na kuingiza utulivu katika ulimwengu wenye msukosuko,” tamko kutoka kwa wataalam wa Serikali ya China, ikionekana kama ni karipio la wazi.

Mataifa yahofia madhara zaidi mabadiliko tabianchi, uviko-19
Bungeni: Kuoana ni baada ya miaka sita - Dkt. Stergomena