Wapenzi wa muziki wa bongo fleva Jina Q chief likitajwa linawakumbusha mbali sana hasa kutokana na nyimbo zake zilizojawa na maudhui maridhawa kabisa.

Kama ukirejea kumbu kumbu kadhaa zinaonyesha msanii huyu alikuwa mfano kwa baadhi ya wasanii wakubwa ka Diamond Plutnumz na wengine bila kusita hadharani walimtaja kama ”role model”.

TBT-Diamond-na-Q-Chief

Miaka kadhaa iliyopita zilizuka habari ya kuwa mwanamuziki huyu aliyejijengea jina na heshima kubwa ya kuwa analalamika Diamond pautnumz anatumia nyota yake kusafiria baada ya kuona mambo hayaendi sawa kwa upande wake.

Hata hivyo Diamond hakuwa nyuma kujibu tuhuma hizo na kusema msanii huyo aache kulalamika zaidi anatakiwa afanye kazi kwa bidii ndipo ataona matunda ya kazi za muziki.

Waswahili wanasema hakuna lenye mwanzo likakosa kesho Q chief amekiri kuwa diamond amefanya kazi nzuri kupeperusha bendera lakini pia amemsaidi hata yeye kupata njia na kutoboa kufika mbali zaidi.

“ametuamsha kuna maboda tikiingia tunapita na kuondokea  i dore him and his work he is made away to other people, i give him a maximum respect matatizo, i adore his work watoto wangu watakuja na hii generation na mwisho wa siku wataweza hata kushoot na kina campuss kwa urahisi zaidi”.

Pamoja na hayo Mkongwe huyo katika kiwanda cha muziki wa bongo fleva amesema  mambo ni mazuri kwa wote wawili na kwamba wanawasiliana mara nyingi na wapo mbioni kufanya kitu cha pamoja.

Video: Katibu Mkuu Tiba Asili Tanzania Apinga Dkt. Mwaka na Wengine Kufutiwa Usajili
Waziri Mkuu, Majaliwa Atoa Wito kwa Wakurugenzi