Qatar imepewa masaa 48 kutimiza masharti 13 iliyopewa na nchi za Kiarabu ikiwemo kukifunga kituo chake cha habari cha Alja Zeera vinginevyo itaongezewa masharti mengine ambayo yataisababishia matatizo makubwa ya mahusiano na nchi hizo.

Aidha, nchi hiyo inatuhumiwa na nchi za kiarabu kuhusika na kudhamini makundi ya Kigaidi ambayo yamekuwa yakihatarisha usalama wa ukanda mzima wa nchi za kiarabu.

Nchi hiyo inaendelea na msimamo wake wa kukataa kuhusika kusaidia makundi ya kigaidi hasa lile la Islamic State ambalo limekuwa likiongoza mashambulizi nchini Syria ambapo mapigano hayo yamedumu kwa muda mrefu.

Hata hivyo, Qatar imewekewa vikwazo vya Kidiplomasia na uchumi kwa muda wa wiki kadhaa na nchi za Misri, Saudi Arabia, Bahrain na umoja wa falme za Kiarabu ambapo imetakiwa kutimiza masharti.

 

?Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Julai 3, 2017
Video: JPM atoa onyo kwa wanasiasa, Bandari Dar sasa habari nyingine