Miezi miwili baada ya kuachiwa kwa albam mpya ya Nicki Minaj ‘Queen’, imefanikiwa kutusua na kufikisha mauzo ya ‘Platinum’, kwa mujibu wa rapa huyo.

Nicki ametoa taaria hiyo nzuri ya kuuza nakala  milioni moja ndani ya kipindi cha miezi miwili, kwa kupost kwenye Instagram kuwashukuru mashabiki wake kwa upendo na namna walivyomuunga mkono.

“#Queen imekuwa albam yangu ya nne kufikisha Platinum nchini Marekani wiki hii. Asanteni sana kwa upendo na kuniunga mkono. Namshukuru kila mmoja ambaye alichangia katika mradi huu kwa namna yoyote. Utukufu ni kwa Mungu,” tafsiri ya alichokiandika Nicki.

Albam hiyo ambayo iliachiwa rasmi Agosti 14 mwaka huu, ilishika nafasi ya pili kwenye Billboard 200 ikiwa na makadirio ya mauzo ya nakala 185,000 katika wiki yake ya kwanza.

Hivi sasa albam hiyo ambayo ndani wamepewa mashavu Eminem, The Weekend na Future inashika nafasi ya 13 kwenye Billboard 200.

Queen ni albam ya nne ya Nicki kufika Platinum, baada ya albam zake za Pink Friday (2010), Pink Friday: Roman Reloaded (2012) na The Pink Print (2014).

Octopizzo aukataa ubunge baada ya kukutana na Bobi Wine
Manara na wengine 18 waachiwa kwa dhamana sakata la Mo Dewji

Comments

comments