Mtandao wa YouTube umefunga Chaneli za mwimbaji wa R&B,  Robert Sylvester Kelly maarufu kwa jina la R. Kelly.

YouTube katika taarifa yake inasema wamelazimika kuzifunga Chaneli za RKellyTV na RkellyVevo zilizokuwa zinamilikiwa na R Kelly kama njia ya kujitenga na udhalilishaji wa kingono alioufanya mwanamuziki huyo.

R.Kelly alihukumiwa hivi karibuni na mahakama moja nchini Marekani na huwenda akakabiliwa na kifungo cha miaka kumi gerezani au kifungo cha maisha.

Mwanamuziki huyo alituhumiwa kutumia umaarufu wake kuwanyanyasa wanawake kingono na kuwaingilia kimwili kwa kutumia ulaghai.

Hata hivyo YouTube imesema mbali na hatua iliyochukua, nyimbo za R Kally  zitaendelea kuonekana katika mtandao huo wa kijamii kwa vile zimepakiwa na watu wengine kutoka sehemu mbalimbali duniani.

“Tunaweza kuthibitisha kuwa tumesimamisha vituo viwili vilivyounganishwa na R. Kelly kulingana na miongozo yetu ya uwajibikaji wa waundaji,” msemaji wa YouTube aliliambia shirika la habari la Reuters.

Kutokana na mwanamuziki huyo kukutwa na hatia ya unyanyasaji kingono kampeni za kutaka nyimbo zake ziondolewe kwenye mitandao ya kijamii kama Youtubemusic, Spotify, AppleMusic, AmazonMusic  zikiendelezwa na watu wanaojiita watetezi wa wanawake.

Mirabaha kuwanufaisha wasanii nchini
Migogoro vyama vya ushirika na wawekezaji Suluhu yapatikana