Mkali wa muziki wa RnB kutoka Marekani R Kelly ameendelea kukana mashtaka yamoyomkabili dhidi ya tuhuma ya za unyanyasaji wa kingono kwa mabinti waliochini ya miaka 18.

R Kelly alipandishwa kizimbani kwenye mahakama ya Cook mjini Chicago June 6, mwaka huu  ambapo makosa manne yalitajwa kupewa daraja X na kuwekwa kwenye kipengele cha makosa ya jinai na huenda akafugwa miaka 30 jela endapo atakutwa na hatia.

Nguli huyo anaekabiliwa na mashtaka 11 ya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo, imeelezwa kuwa ameendelea kukana mashtaka ambayo yalifunguliwa siku ya alhamisi May 30, 2019.

Ikumbukwe kuwa R Kelly, alikabiliwa na mashtaka 10 ya uyanyasaji wa kingono mwanzoni mwa mwaka huu ambapo alikana kuhusika na vitendo hivyo na kuachiwa huru kwa dhamana zaidi ya shilingi millioni 200 za kitazania.

 

 

 

Mwadini ajitia kitanzi Azam fc
Mwalimu afariki baada ya kunywa gongo

Comments

comments