Menu

R.Kelly amlilia Jaji amtoe jela, ahofia virusi vya Corona

10 months ago Comments Off on R.Kelly amlilia Jaji amtoe jela, ahofia virusi vya Corona

Robert Kelly maarufu kama R Kelly amemuomba Jaji amuachie huru kutoka katika Gereza la Metropolitan Correctional Center huko Chicago nchini Marekani akihofia kupata maambukizi ya Virusai vya Corona.

Hivi karibuni, Jopo la Majaji wa Chicago walionesha nia ya kumuachia kwa dhamana msanii huyo, lakini jaji wa New York akapigilia msumari kuwa msanii huyo abaki gerezani.

Kwa mujibu wa CNN, barua ya maombi hayo iliyowasilishwa mahakamani hapo na wakili wake, Steven Greenberg ilieleza kwamba mteja wake huyo mwenye miaka 53 yupo katika hatari ya kupata maambuziki hayo.

Barua hiyo ilieleza hatari iliyo katika gereza la Metropolitan Correctional Center, kuwa hakuna sabuni na vitakasa mikono vya kutosha na watu wengi wanawekwa katika selo ndogo mbili, hivyo kusababisha msongamano.

“Katika vyoo na mabafu vya wageni hapa MCC, hakuna sabuni wala karatasi laini za msalani, hivyo inakuwa ngumu kuosha mikono kabla ya kuingia ndani kuona wafungwa na mahabusu,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

Mfalme huyo wa RnB mapema Julai, 2019 alikamatwa kwa mara ya pili na Idara ya Polisi ya New York kwa tuhuma za kuwasafirisha wanawake kwa ajili ya kuwatumikisha kingono, huku akituhumiwa kuhusikana makosa 10 ya ngono.

Mei alikamatwa tena na kushtakiwa kwa tuhuma za kuhusika na makosa 11 ukiachilia makosa 13 ya awali ya unyanyasaji wa kingono ambapo kati ya makosa hayo yalikuwemo yanayohusisha kifungo cha hadi miaka 30 jela.

 

Mmarekani aliyekwepa karantini akamatwa Dodoma
Meya wa Ubungo atangaza kung’atuka udiwani

Comments

comments

%d bloggers like this: