Mwanamuziki kutoka Nigeria maarufu kama Davido bado anaendelea kufanya vizuri katika muziki wake, staa huyo ambaye aliachia wimbo wake wa ‘IF’,  bado unafanya vizuri katika chati za muziki ndani na nje ya Afrika, hayo yamethihirishwa wazi na msanii mkongwe wa RnB kutoka Marekani R.Kelly baada ya kuonekana akipost katika mitandao ya kijamii kuwa amefanya remix cover ya wimbo wa If na Davido.

Davido ametambulika vizuri na R.Kelly  kupitia wimbo wa ‘If’ ambapo kupitia ukurasa wa Instagram wa R.Kelly akiwa katika location ya Nigeria ameandika na kusema imemtumia muda wake mwingi  kufanya kitu kwenye wimbo wa ‘If’ ambacho ni Remix iliyoingia mtandaoni mapema jana.

Image result for R.kelly IF

Hata hivyo Davido anaendelea na ziara yake ya Dunia ‘The 30 BILLION WORLD TOUR’ ambapo baada ya show yake ya Djibouti anajipanga kutumbuiza tena tarehe 30 mjini Stockholm nchini Uswidi(Sweeden.)

Makonda awatoa dinner WCB
Wanne Kutoka Tanzania Bara Na Zanzibar Kusajiliwa Mwadui FC