Kiungo wa Paris Saint-Germain, Adrien Rabiot, ameweka wazi kwamba wachezaji wenzake wawili, Neymar na Kylian Mbappe wanapendelewa zaidi klabuni hapo, lakini akasema kuwa kwake hilo siyo tatizo na wala hamuonei wivu mtu yeyote.

Kauli hiyo inakuja baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa Neymar ameruhusiwa kutumia begi lenye nembo yake wakati wachezaji wengine wakitakiwa kutumia bidhaa za PSG pekee.

Rabiot pia amefichua kuwa wachezaji wa PSG wameambiwa wakiwa mazoezini wasimkabe Neymar kwa nguvu ili asiumie, kitendo kinachodhihirisha kuwa nyota huyo wa Brazil anadekezwa.

Kauli ya Rabiot inajazia taarifa zilizowahi kusambaa mwezi Oktoba mwaka jana zikidai kuwa wachezaji wa PSG wamechoshwa na vitendo cha upendeleo wa wazi kwa Neymar.

Inaelezwa kuwa PSG wamekuwa wakimtunza Neymar kutokana na kumsajili kwa dau kubwa lililoweka rekodi mpya ya dunia, hivyo wanapambana kuhakikisha wanamtumia kurudisha fedha zao.

 

Ligi ya Mabingwa Ulaya kuendelea leo
Talgwu: Alichofanya Makonda ni kitendo cha kinyama

Comments

comments