Mabosi FC Bayern Munich wanafikiria kumsajili kiungo wa West Ham na England, Declan Rice mwenye umri wa miaka 24, wakati wa usajili wa majira ya Kiangazi.

Munich imedhamiria kweli kumsajili Rice kwa sababu inaamini itamtumia kwa muda mrefu kutokana na umri wake.

Rice ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2024, amekuwa akihusishwa na timu nyingi za Ligi Kuu ya England ikiwemo Arsenal.

Licha ya wingi wa timu zinazohitaji huduma yake, timu itakayofanikiwa ni ile itakayokubali kulipa zaidi ya Pauni 90 milioni inayotakiwa na West Ham ili kumuuza kiungo huyu.

Hadi sasa hakuna timu iliyoonekana kuwa tayari kulipa kiasi hiki cha pesa hali inayosababisha dili kuwa gumu.

Hata hivyo matumaini ya timu nyingi ni kadri muda unavyozidi kwenda ndio West Ham itazidi kulegeza na kukubali kumuuza ile kwa pesa pungufu zaidi ya wanayoitaka hivi sasa lakini hilo halionekani kwani bado wameendelea kukaza.

Msimu huu Rice amecheza mechi 48 za michuano yote, amefunga mabao matano na kutoa asisti nne.

Homa ya kuvuja damu mwilini yauwa mmoja, tahadhari yatolewa
Wanajeshi wa Urusi waharibu vifaa vya Marekani Ukraine