Mwanafunzi mmoja aliyefahamika kwa jina la Abdul Athumani Masamba wa kidato cha tatu wa shule ya sekondari Mikindani amefariki dunia na wengine 32 kujeruhiwa kwa kupigwa na Radi walipokuwa Darasani wanasoma.

Radi hiyo ilitokea machi tano mwaka huu majira ya saa nne asubuhi katika shule ya sekondari Mikindani Manispaa ya Mtwara ambapo ilijeruhi wanafunzi wa kidato cha tatu ‘’ A ‘’ waliokuwa darasani wakiendelea na masomo.

Wakizungunza kwa shida baadhi ya majeruhi hao wakati wakipatiwa matabu katika kituo cha afya cha Mikindani na Hospitali ya Rufaa Mkoani humo (Ligula) wamesema kuwa waliona mwanga mkali uliombatana na muungurumo mkali wa Radi ,na baada ya mshuko walijaribu kujificha china ya meza lakini hali  hiyo haikuwasaidia.

Ninacho kumbuka Mwalimu wetu wa geography alikuwa anafundisha mada ya Map na alipokuwa anamalizia akatoa nafasi ya sisi kuuliza maswali ghafla ukapiga mwanga mkali ulioambatana na mngurumo wa Radi tukajificha chini ya meza zetu lakini kuna mwezenzetu mmoja akaangunga chini na akalala chali’.Amesema Omary Mhidini Mmoja wa wanafunzi aliyejeruhiwa

Aidha, Darasa hilo la Kidato cha Tatu “A” lilikuwa na jumla ya wanafunzi 33 ambapo mwanafunzi mmoja aliefahamika kwa jina la Abdul Athumani Masanga alifariki Dunia akiwa njiani alipokuwa anapelekwa hopitali kwa ajili ya matibabu .

Mmoja wa wazazi wa mwanafunzi aliyejeruhiwa na Radi aliyefahamika kwa jina Ahmadi Kisewa amesema kuwa hali hiyo si kawaida kutokea ingawa kuna matukio tofauti yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika shule hiyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Maafa wilaya ya Mtwara ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo, Evod Mmanda amesema kuwa amepokea kwa masikitiko juu ya tukio hilo huku akiwasihii wazazi na walezi kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki kigumu kwani janga hilo ni pigo kwa wilaya nzima.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo Dkt. Lobikieki Kissambu amesema kuwa hali ya Majeruhi waliopokelewa hospitalini hapo ambapo amedai wamepokea jumla ya wanafunzi 24 na wawili kati yao walipata matibabu na kuruhusiwa huku 22 bado wanaendelea kutibiwa

Video: Mgonjwa wa Ukimwi aripotiwa kupona, Kusuka, kunyoa rufani ya Mbowe
Typhod na magonjwa ya tumbo yawatesa wananchi Wanging'ombe

Comments

comments