Mwanamke mmoja na watoto wake wawili wapoteza maisha Jumamosi iliyopita baada ya kupigwa na radi wakati katika kijiji cha Kamujwa nchini Kenya.

Baba wa familia hiyo, Gichuri Mwamba amesema kuwa mkewe alikuwa ametoka kwenye mkutano muda mfupi kabla ya kukumbwa na tukio hilo baya.

Mwamba ambaye hakuwa nyumbani kwake wakati huo, alisema kuwa mkewe alikuwa na watoto wanne ndani ya nyumba yao majira ya saa mbili usiku wakati tukio hilo linatokea.

Citizen ya Kenya imeripoti kuwa Mamlaka ya hali ya hewa imewataka wananchi kujitahidi kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua kubwa ambazo zimeanza kushuhudiwa katika maeneo ya Embu, Tharaka Nithi na Meru.

Video: Moto wateketeza soko la Mbagala
Video: Mangula awachana wanasiasa wachochezi, Mbowe alazwa awekwa oxygen