Rafa Benitez amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya Everton ambayo inatajwa kuwa mbioni kumtimua kazi meneja wao wa sasa Ronald Koeman, kufuatia matokeo mabaya yanayoendelea kuwaandama.

Benitez alikua wa kwanza kwenye orodha ya mameneja wanaopigiwa chepuo kuchukua nafasi ya ukuu wa benchi la ufundi huko Goodison Park, kutokana na kuwa na uzoefu wa kutosha katika ligi ya England.

Benitez, mwenye umri wa miaka 57, ametangaza msimamo huo, kwa kuamini bado ana nafasi ya kuendelea kudhihirisha ubora wake akiwa na kikosi cha Newcastle Utd, ambacho alikirejesha ligi kuu msimu uliopita kikitokea ligi daraja la kwanza.

“Kazi yangu kubwa ni kuangalia namna nitakavyoweza kutimiza majukumu yangu ipasavyo, sitilii maanani taarifa zinazo zungumzwa kuhusu mimi.

“Watu wanaweza kuzungumza lolote walitakalo, tena kwa wakati wowote ule, lakini msimamo wangu utaendelea kubaki kama nilivyosema, kazi yangu ni kuangalia namna ya kutimiza majukumu yangu.” Alisema Benitez

Benitez anaendelea kukumbuka ka kazi nzuri aliyoifanya akiwa na liverpool mwaka 2005, na kufikia mafanikio ya kutwaa ubingwa wa barani Ulaya kwa kuifunga AC Milan.

Waziri Kigwangalla kukutana na wadau wa maliasili na utalii
Rabah Madjer abebeshwa zigo AFCON 2019