Aliyewahi kuwa meneja wa majogoo wa jiji Liverpool, Rafael Benitez ametoa mtihani mzito kwa viongozi wa klabu hiyo ya Anfield, baada ya kuonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi na klabu ya Newcastle Utd, Georginio Wijnaldum.

Benitez ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Newcastle Utd, ambacho msimu wa 2016/17 kitashiriki ligi daraja la kwanza nchini England, ameutaka uongozi wa klabu hiyo kukubali kumuachia kiungo kutoka nchini Brazil, Lucas Leiva ili awe sehemu ya makubaliano ya kuondoka kwa Wijnaldum.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania ameonyesha kuhitaji huduma ya Leiva kikosini mwake, na amedhamiria kutumia mwanya huo kumpata kirahisi ili kutimiza lengo lake kwa msimu ujao wa ligi daraja la kwanza.

Hata hivyo tayari klabu ya Liverpool ilikua imeshajinasibu kutoa kiasi cha pauni milion 25 kama ada ya uhamisho wa Wijnaldum, lakini kwa sharti hilo hawana na budi kujipanga upya ili kuona kama wataafiki kumuachia mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 29.

Leiva alisajiliwa na Benitez mwaka 2007 akitokea kwenye klabu ya Grêmio ya nchini kwao Brazil, na alionekana kushabihiana na mfumo wa meneja huyo kwa kucheza soka la kujiamini wakati wote.

Juventus FC Waigomea Man Utd
Maji yawafika kooni viongozi CCM waliokwepa kumpokea Magufuli akiomba udhamini