Hatimae Rafael Benitez, amefikia makubaliano na uongozi wa klabu ya Newcastle United ya kuendelea kubaki klabuni hapo kwa lengo la kukinoa kikosi cha klabu hiyo ambacho msimu ujao kitashiriki ligi daraja la kwanza nchini Engalnd.

Benitez, amefikia makubaliano na uongozi wa klabu hiyo kwa kukubali kusaini mkataba wa miaka mitatu ambapo inaaminiwa atafanikisha azma ya kuirejesha The Magpies katika mshike mshike wa ligi kuu ya soka nchini England ndani ya muda huo.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania, alisaini mkataba wa muda mfupi kwa ajili ya kukinoa kikosi cha Newcastle Utd, ambapo makubaliano hayo yalimalizika baada ya msimu wa 2015-16, kufikia kikomo majuma mawili yaliyopita.

Dhamira kubwa ya uongozi wa Newcastle Utd pamoja na Benitez ilikua ni kuhakikisha anafanya manusura ya kutoshuka daraja, lakini kwa bahati mbaya zoezi hilo halikufanikiwa mwishoni mwa msimu.

Benitez alikabidjhiwa kikosi cha klabu hiyo ya St James Park, baada ya kutimuliwa kwa aliyewahi kuwa meneja wa timu ya taifa ya England, Steve McClaren mwezi Machi mwaka huu.

Arsenal FC Wathibitisha Usajili Granit Xhaka
Video: Jambo hili lisipo pata majibu leo Mh. Waziri nakwambia hapahapa nakufa na wewe - Doto Biteko

Comments

comments