Aliyekua meneja wa klabu ya Real Madrid, Rafael Benitez anategemea kurejea katika ligi kuu ya soka nchini England, kufuatia jina lake kutajwa katika sehemu ya vikao vya viongozi wa klabu ya Newcastle Utd.

Viongozi wa Newcastle Utd wanafikiria kubadili wahusika katika benchi la la ufundi kufuatia mambo kuwaendea kombo, ambapo mpaka sasa hawafahamu hatma yao kama wataendelea kusalia ligi kuu ya EPL, ama kushuka daraja kutokana na mwenendo wa kikosi chao.

Newcastle ipo nafasi ya pili kutoka chini, na kama mambo yataendelea kuwa hivyo hadi mwishoni mwa msimu huu, hakuna budi kwao kurejea ligi daraja la kwanza kwa msimu wa 2016-17.

Taarifa zinaeleza kwamba Rafael Benitez anategemea kukutana na uongozi wa klabu ya Newcastle United mwishoni mwa juma hili, ili kukamilisha baadhi ya mambo, kabla ya kuchukua nafasi ya meneja Steve McClaren ambae atafukuzwa kazi wakati wowote kuanzia sasa.

Imebaki michezo michache hadi ligi itakapomalizika na Newcastle Utd, bado wanahaha ili kubaki kwenye Primer League msimu ujao.

Ziara ya Zambia Yaanza Kuzaa Matunda Azam FC
Picha: Bibi harusi Ampiga bwana harusi mbele ya waalikwa, Siku ya wanawake duniani