Beki wa kati kutoka nchini Ufaransa na klabu bingwa barani Ulaya (Real Madrid) Raphael Varane, amevuruga mipango ya usajili ya Jose Mourinho.

Varane amevuruga harakati za meneja huyo kutoka nchini Ureno, baada ya kuweka bayana mustakabali wake wa kuendelea kucheza soka Santiago Berbnabeu kama mkataba wake unavyomruhusu.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 23, amekua katika rada za Jose Mourinho tangu alipotua Old Trafford mwezi Julai mwaka huu, lakini kwa kauli aliyoitoa ya kutokua tayari kuihama Real Madrid imemaliza rasmi harakati za mreno huyo.

“Katika kipindi hiki, sina pengine pa kwenda zaidi ya kumalizia soka langu nikiwa na Real Madrid,” Alisema Varane.

“Mambo yanakwenda kwa kasi kubwa katika tasnia ya mchezo wa soka, na mimi sitaki kujipotezea muda wa kuhangaika kuhama hapa na pale, zaidi ya kutambua nilipo kwa sasa pananitosha.

“Ninajihisi furaha wakati wote tangu niliposajiliwa hapa mwaka 2011. Na niwaeleze wanaotamani kunisajili, kwa kusema itakua vigumu kwao kuning’oa Real Madrid.

Varane anatazamwa kama mrithi mkubwa katika safu ya ulinzi la Real Madrid baada ya Pepe na Sergio Ramos ambao huenda wakaamua kuondoka klabuni hapo wakati wowote, kutokana na kuwa na umri mkubwa.

Jose Mourinho alimsajili Varane mwaka 2011 wakati akiwa meneja wa klabu ya Real Madrid, akimtoa nchini kwao Ufaransa ambapo alipokua akiitumikia klabu ya Lens.

Meya Seongnam Kusapoti TFF
Azam U-20 Kuanza Na Mbao Ligi Ya Vijana Kesho