Mshambuliaji wa klabu bingwa nchini England Man City Raheem Sterling ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa, ambacho kimeanza kambi ya kujiandaa na mchezo wa ligi ya mataifa ya Ulaya (UEFA Nations League) dhidi ya Hispania utakaochezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Wembley.

Taarifa ya chama cha soka nchini Engalnd (FA) imeeleza kuwa mshambuliaji huyo ameondolewa kikosini kufuatia majeraha ya mgongo yanayomuandama.

Sterling ambaye tayari ameshaitumikia klabu yake katika michezo mitatu ya ligi msimu huu, alibainika kuwa na majeraha hayo baada ya kufanyiwa vipimo saa kadhaa baada ya kuwasili kambini.

Hata hivyo kocha mkuu wa England Gareth Southgate, amesema hatoajaza nafasi ya mshambuliaji huyo kwa kumuita mchezaji mwingine, na badala yake ataendelea na wachezaji waliosalia kikosini.

Mbali na mchezo dhidi ya Hispania siku ya jumamosi, England itacheza dhidi ya Uswiz siku ya jumanne ya juma lijalo kwenye uwanja wa King Power.

Uwekezaji kutoka China kuifikisha Tanzania uchumi wa kati
Jean- Pierre Bemba akosa sifa za kugombea Urais Congo DRC

Comments

comments