Serikali ya Singapore imesema inampango wa kugawa pesa zilizobaki katika bajeti ya mwaka 2017 kuwapa raia wake wote wenye kipato cha kuanzia Dola ya Singapore 28,000 hadi Dola 100,000 kwa lengo la kuongeza kipato kwa wananchi wake na kuleta maendeleo.

Takribani watu milioni 2.7 wenye umri wa zaidi ya miaka 21 wataongezewa kiwango cha Dola 100 hadi 300 katika mishahara yao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha wa Singapore, Heng Swee Keat wakati akiwasilisha Bungeni Bajeti, ambapo amesema bonasi hiyo ni dhamira ya muda mrefu ya Serikali ya kugawana matunda ya maendeleo na raia wake.

Waziri huyo ameongezea kuwa uamuzi huo umefikiwa mara baada ya kuona Bajeti iliyopangwa na kutolewa kwa mwaka 2017 ilikuwa kubwa na kiwango kikubwa cha pesa kimebakia.

Mnamo mwaka 2011, watu wazima nchini humo waliokuwa na kipato cha mwaka cha hadi dola 30,000 iliwalipa dola 800.

 

Sugu, Masonga wafungwa miezi mitano jela
Hatma ya 'Sugu' kujulikana leo