Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imetoa hati ya kukamatwa raia wanne wa msumbiji na mmoja wa Afrika Kusini ili wafikishwe kizimbani na kuunganishwa katika mashtaka ya kumteka mfanyabiashara maarufu nchini Mohammed Dewji.

Hati hiyo imetolewa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya wakili wa Serikali, Wankyo Simon kuomba Mahakama itoe hati hiyo.

Wakili Wankyo amewataja wanaotafutwa ili kuunganishwa na mshtakiwa Mousa Twaleb, ni raia wa Msumbiji, Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issa Tomo, Zacarious Junior na raia wa Afrika kusini Phila Tshabalala.

Washtakiwa hao wanatakiwa kuunganishwa katika shataka la pili na shtaka la tatu, ambapo shtaka la kwanza linamkabili Twaleb (dereva), ambaye anadaiwa kujihusisha na genge la uhalifu, kati ya Mei 1 na Oktoba 2018.

Sakata la pili ni la kujihusisha na genge la uhalifu linalowakabili wote, na la tatu ni washtakiwa wote wanadaiwa kumteka nyara mfanyabiashara Dewji, Oktoba 11, 2018 katika Hoteli ya Colleseum wilayani Kinondoni kwa nia ya kumhifadhi kwa siri kinyume cha sheria.

Pinda awashukia ‘akina Membe’
Kamanda Muroto awatahadharisha matapeli jijini Dodoma

Comments

comments