Mtu mmoja raia wa Ufaransa ameanza safari ya kuvuka bahari ya pili kwa ukubwa duniani, Atlantiki, kwa kutumia pipa kubwa aliloliunda mwenyewe.

Jean-Jacques Savin, mwenye umri wa miaka 71, ameanzia safari hiyo kutoka mji wa El Hierro uliopo kwenye visiwa vya Canary nchini Uhispania na anataraji kufika visiwa vya Caribbean ndani ya miezi mitatu.

Aidha, Pipa hilo linategemea nguvu ya msukumo ya mawimbi pekee kufanikisha safari, ambapo ndani ya pipa hilo kuna sehemu ya kulala, jiko na stoo ya kuhifadhi vitu.

“Hali ya hewa ni nzuri, naenda kwa kasi ya kilomita mbili mpaka tatu kwa saa, utabiri wa upepo ni mzuri kwangu,”amesema  Savin alipokuwa akifanya mahojiano na shirika la habari la AFP

Hata hivyo, Savin ni mwanajeshi mstaafu aliyekuwa akiruka kwa parashuti (askari wa mwamvuli) na pia ameshawahi kufanya kazi kama mlinzi wa mbuga na rubani,

Maafisa wa Indonesia waonya kuhusu mlipuko wa Volcano
Live: Rais Magufuli akutana na viongozi wa TUCTA, NSSF, PSSSF na SSRA kuhusu KIKOKOTOO