Mgombea wa urais wa muungano wa Azimio la Umoja One nchini Kenya, Raila Odinga ameongeza sera katika kampeni zake za kugombea urais wa nchi hiyo akidai kuwa hatapiga marufuku uagizaji wa mitumba iwapo atachaguliwa Agosti 9.

Raila ambaye alikutana na wawikilishi wa soko la Gikomba siku ya Ijumaa, Juni 24, alisema kuwa serikali ya Azimio itashirikiana na wafanyabiashara kuhakikisha kuwa matajiri wanaotumia njia za mkato kujitajirisha zaidi kupitia kwa biashara hiyo watakabiliwa.

Wafanyabiashara hao walimwambia Raila kuwa wanategemea mitumba kulisha familia zao na kwa hivyo wanahofia kile kinachoweza kutokea iwapo itapigwa marufuku.

“Sisi hatuwezi tukataka hayo matamshi yaendelee, hiyo siasa ya mitumba iendelee. Mitumba kwetu ni chakula, tukinyang’anywa mitumba tumenyang’anywa chakula. Mitumba ikitumiwa kisiasa ni sisi tunaharibiwa biashara yetu,” mmoja wa wafanyabiashara hao alisema.

Kiongozi huyo wa chama cha ODM aliwahakikishia wafanyakazi kuwa serikali yake itashirikiana nao kuimarisha soko lao pamoja na kuanzisha kampuni za kutengeneza nguo.

Mahujaji kuchanjwa tena COVID
NHIF yasitisha huduma