Kiongozi Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga, Jumamosi, Januari 15, atakuwa katika kaunti ya Kiambiu kuzindua rasmi kampeni za kuwania urais nchini Kenya.

Raila atakuwa katika uwanja wa Thika, kaunti ya Kiambu ambapo ataanza safari yake ya kutafuta kura za kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.

Thika ina umuhimu kwa Raila kwa sababu aliwahi kuzindua kampeni humo mwaka 2005 kuhusu mabadiliko ya katiba na ni muhimu kwake kwani ndio nyumbani kwa Rais Uhuru ambaye walifanya mkataba wa kisiasa wa handisheki naye.

Akiongea na vijana Jumanne Januari 11 wakati alipokutana na familia za waliokuwa wafungwa wa kisiasa, Raila alisema mkutano huo wa Thika Jumamosi ndio utakuwa wa kwanza.

“Jumamosi, Azimio la Umoja watakuwa Thika. Huu ndio utakuwa mkutano wa kwanza wa Azimio 2022, Barabara zote zitaelekea Thika ambapo tutaongea na wakazi kutoka Murang’a na Kiambu,” alisema kiongozi huyo wa ODM.

Watu wa karibu wa Raila walisema wamejipanga na kampeni zake zitakuwa kama zile za 2002 zilizowika na kuondoa Kanu mamlakani.

Gavana Nderitu Muriithi ambaye anaongoza kampeni za Raila alisema wakati huu kiongozi huyo atapata asilimia 60 ya kura za Mlima.

Handisheki kati ya Raila na Uhuru imempa nafasi ya kupenya eneo la Mlima Kenya na sasa kinachosubiriwa ni kuona ni nani atakuwa mgombea mwenza wake.

Viongozi kadhaa wa Mlima Kenya kama vile Waziri Peter Munya na Peter Kenneth wamekuwa wakijipanga nyuma ya ‘Baba’ akitajwa Raila.

Wadadisi na wataalamu wa masuala ya kisiasa wametangaza kuwa kinyang’anyiro cha 2022 wagombea wakuu ni wawili ambao ni DP Ruto na Raila Odinga.

Mwanahabari wa marekani apata umaarufu Kenya kutokana na giza.
Kinachosabisha ndoa za "Babu na Mjukuu"