Kiongozi Muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga amewataka Wakenya kususia kulipa kodi ambayo imeongezeka maradufu tangu kuingia kwa utawala wa Rais William Ruto, huku akitaka matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana 2022 yakaguliwe.

Odinga, ameyasema hayo wakati akiongea na wafuasi wake jijini Naorobi na kuongeza kuwa, Wakenya wamekuwa wakiishi maisha magumu tangu kuingia madarakani kwa Rais Ruto, kitu ambacho si sawa.

Raila Odinga katika moja ya mikutano yake nchini Kenya. Picha ya KDN.

Kauli ya Odinga, inakuja mara baada ya Rais Ruto kusema hatokubali watu wachache wakwamishe utendaji wa kazi wa serikali yake ya kuwahudumia Wakenya, na kwamba hatua stahiki zitachukuliwa kwa wahusika.

Mkutano huo, ulihudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Muungano wa Azimio la Umoja, akiwemo Martha Karua, Kalonzo Musyoka, na kiongozi wa chama cha Roots George Wajackoya huku akisema kwa sasa upinzani unataka matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita yakaguliwe upya na kutangazwa kwa Wakenya.

Wengine saba wauawa kwa risasi shamba la uyoga
Vijana wabuni mradi mabegi ya Nishati jua