Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF), nchini Kenya limetoa wito kwa Serikali itakayoingia madarakani mara baada ya uchaguzi wa mwezi Agosti, kutoa kipaumbele kwa hifadhi ya jamii ikiwemo kupatia fedha familia zilizo hatarini na hali ya umaskini.

UNICEF, imetoa wito huo hii leo Julai 25, 2022 wakati ambapo mradi wake wa majaribio wa kuzipatia fedha famiilia maskini zenye watoto umeanza kuzaa matunda.

Mgombea wa Urais nchini Kenya, Raila Odinga.

Mkazi wa Kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambaye ni bibi na mlezi wa wajukuu watano na binti yake kiziwi ni mmoja wa wanufaika wa mradi wa UNICEF aliyepata fedha za kaya maskini, amesema kila mwezi hupatiwa dola 17 ili kuweza kulea wajukuu zake akiwemo Alice mwanafunzi wa darasa la saba.

Amesema, ukosefu wa fursa za ajira na changamoto itokanayo na janga la Uviko-19 ambapo umesababisha hali kuwa mbaya zaidi na watoto kushindwa kwenda shule, huku akiunga mkono kauli ya UNICEF juu ya kuzipa kipaumbele kaya masikini.

Awali akiongea jijini Nairobi, afisa wa UNICEF Kenya, Susan Momanyi anasema, “hapa Kenya kaya milioni 1.4 zimeandikishwa kwenye mradi wa hifadhi ya jamii, na hivoy kuacha takribani watoto milioni 12 wanoahitaji huduma hiyo. 

Momanyi amezidi kufafanua kuwa, “Ndio  maana UNICEF inatoa wito kwa serikali ijayo ya Kenya kuongeza bajeti kwenye hifadhi ya jamii kwa asilimia 1.7 ya pato lake la ndani, kiwango ambacho ni sawa na nchi zingine za kipato cha kati ili kila mtoto anufaike.”

30 wafariki ajali basi la Morden Coast
WHO yataka juhudi kupunguza vifo majini