Chama tawala cha Unity nchini Liberia kimemtimua Rais anayemaliza muda wake, Ellen Johnson Sirleaf kwa tuhuma za kutomuunga mkono mgombea mwenza ili arithi kiti chake cha urais.

Chama cha Unity kinamtuhumu Ellen kwa kuwahamasisha wananchi kutompigia kura mgombea ambaye alikuwa Makamu wa Rais, Joseph Boakai.

Aidha, chama hicho kinamtuhumu kwa kukiuka Katiba kwa madai ya kumfanyia kampeni George Weah, ambaye aligombea kupitia chama cha Coalition for Democratic Change, na kuibuka mshindi.

Weah ambaye ni mwanasoka nyota wa zamani, ataapishwa rasmi tarehe 22 mwezi huu ikiwa ni mara ya kwanza Liberia inashuhudia mabadiliko ya uongozi kwa njia ya amani tangu mwaka 1944.

Rais wa Palestina Abu Mazen azidi kumpinga vikali Trump
Video: Askofu Kakobe aelezea alivyohojiwa na TRA, Neema tano ziara ya Kagame Tanzania