Mahakama Kuu ya Marekani, imeweka vikwazo kwa Mamlaka ya Wakala wa Ulinzi wa Mazingira ili kuzuia utoaji wa kaboni kutoka kwa mitambo ya kuzalisha umeme, hali inayomuweka Rais Biden katika ugumu wa kufikia malengo aliyojiwekea katika sekta ya Nishati.

Vikwazo hivyo, vimejumuisha na uhaba wa nishati Duniani kote ikiwemo siasa za ndani, uamuzi unaofanya iwe vigumu kwa Rais Biden kufikia malengo yake katika masuala ya hali ya hewa.

Jaji Mkuu wa Mahamaka Kuu ya jijini New York, John Roberts amesema mabadiliko ya hali ya hewa ni kiasi kidogo cha madhara kilichoangaliwa na kwamba Congress haikuipa E.P.A. mamlaka ya kudhibiti eneo la nishati.

Hivi ni jinsi hali ilivyokuwa nje ya Mahakama ya Juu, baada ya kutolewa kwa uamuzi huo Julai 2, 2022.

Wataalam wananya juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na katika pingamizi hili majaji watatu wa Mahakama hii walisema uamuzi huo umeondoa E.P.A. ya nguvu ya kukabiliana na changamoto kubwa zaidi ya mazingira ya wakati wetu,” amesema Jaji Robert.

Hata hivyo, wataalamu hao wanasema uamuzi huo utafanya iwe vigumu kwa Rais Biden kihisabati katika kutimiza ahadi ya kampeni ya kupunguza uchafuzi wa Marekani kwa nusu ifikapo mwisho wa muongo.

Athari za uamuzi huo, zinaweza kuenea zaidi ya sera ya mazingira na kuwarahisishia wamiliki wa biashara kupinga kanuni nyingi.

IOM yawalilia waliokufa kwa kiu jangwani

Mahakama ya Juu pia iliunga mkono juhudi za Biden kukomesha mpango unaoitwa Baki Mexico, sera ya enzi ya Trump ambayo inawahitaji wahamiaji wanaotafuta hifadhi kubaki Mexico wakati kesi zao zikisikilizwa.

Miongoni mwa majaji wanaosikiliza kesi hiyo ni pamoja na Ketanji Brown Jackson, ambaye ni mwanamke wa kwanza Mweusi kuhudumu katika Mahakama akichukua nafasi ya Jaji Stephen Breyer, aliyestaafu rasmi hii leo July 3, 2022.

Wakutwa na hatia kwa kusaidia mauaji
Nyuki wapambana na askari kuwalinda wazawa