Serikali ya nchi ya Equatorial Guinea imetia saini kubatilisha hukumu ya kifo, itakayoanza kutumika ndani ya siku 90 kufuatia kuchapishwa kwake katika jarida rasmi la serikali na ambayo hapo awali iliyoidhinishwa na bunge.

Sheria hiyo mpya iliyotiwa saini na Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, imepongezwa na mtoto wake ambaye anahudumu kama makamu wa rais wa nchi hiyo akisema ni uamuzi wa kihistoria, kupitia chapisho lake la mtandaoni kwenye Twitter.

Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo. Picha na News 24.

Utekelezaji rasmi wa mwisho katika nchi hiyo ndogo barani Afrika, ulifanyika mwaka 2014 huku mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa na Umoja wa Mataifa mara kwa mara wakishutumu serikali kwa matukio ya kutoweka kwa watu, kuwekwa kizuizini kiholela na kuteswa.

Guinea ya Ikweta, chini ya Rais wake Teodoro Obiang (80), inaifuata Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo ilipitisha sheria hiyo Mei 2022, Chad mwaka 2020 na Sierra Leone mwaka jana 2021, kupiga marufuku adhabu ya kifo katika bara la Afrika.

Ruto kuhutubia Baraza kuu la Umoja wa Mataifa
Wafafanua Viongozi kutumia basi moja mazishi ya Malkia