Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi amesema taifa limekumbwa na msiba mkubwa kutokana na kifo cha kiongozi wao Afonso Dhlakama aliyefariki dunia Alhamisi ya Mei 3, 2018 akiwa na umri wa miaka 65 katika mji wa Gorongosa kutokana na ugonjwa wa kisukari.

Kiongozi huyo wa kundi la zamani la waasi la Rebel Mozambique National Resistance (REMONA) aliongoza vita vya msituni tangu Msumbiji ilipojinyakulia uhuru mwaka 1975 hadi makubaliano ya Amani yalipofikiwa mwaka 1992.

Katika taarifa iliyotolewa na ikulu ya Msumbiji Ijumaa imeeleza kuwa Rais Nyusi amesema ni pigo kubwa kwake kwani walikuwa wamefikia makubaliano ya hivi karibuni ya kutatua matatizo ya nchi, kuleta mabadiliko ya katiba na kumaliza uhasama wa miaka mingi kati ya chama tawala cha Frelimo na Renasmo.

Dhlakama alishindwa katika kila uchaguzi wa urais alioshiriki tangu mwaka 1992, na alikuwa anajitayarisha kugombania kiti cha urais kwa mara nyingine 2019 dhidi ya Rais Nyusi.

Alichukuwa uamuzi huo baada yakufikia makubaliano mapya ya kusitisha mapigano mwaka 2016 na kukubali kurudi katika jukwa la kisiasa. Mashirika ya kutetea haki za binadamu wanamlaumu kwa kusababisha mauaji na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika ngome yake kati kati ya Msumbiji.

Video: JPM amkabidhi mwanafunzi milioni 3 za ujenzi wa vyoo shuleni kwao
Video: Hali yazidi kuwa tete jijini Dar baada ya mvua kubwa kunyesha