Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte amewaja hadharani watu 150 wakiwemo majaji, Meya, wabunge, polisi na wanajeshi ambao wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini humo.

Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte

Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte

Rais Duterte ametaja orodha hiyo wiki iliyopita kupitia kituo cha runinga cha Taifa hilo akiwataka kujisalimisha kabla hajawachukulia hatua kali ikiwa ni sehemu ya operesheni maalum ya vita dhidi ya wauza dawa za kulevya.

Amewataka walinzi wote wa Serikali waliokuwa wanawalinda viongozi hao wote aliowataja kwenye orodha hiyo kuondoka mara moja na kuacha kuwalinda. Pia, ameagiza watu hao kunyang’anywa leseni ya umiliki silaha.

“Wanajeshi wote na polisi ambao walikuwa wanawalinda watu hao, nawapa saa 24 kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi vinginevyo nitawaondoa kwenye majeshi,” alisema Rais Duterte kwenye hotuba yake.

“Hakuna michakato kwenye mdomo wangu. Hamuwezi kunizuia na siogopi hata kama mnasema naweza kuishia jela,” alisisitiza.

Katika orodha ya majina hayo, wamo viongozi ambao walikuwa wakifahamika kama marafiki wa Rais huyo. Majina hayo yaliidhinishwa na Mamlaka lakini bado hayakuwa na maelezo yote kuhusu ushiriki wa watu hao kwenye biashara ya dawa za kulevya.

Joseph Msukuma ang’aka kulipwa na Lowassa
BAVICHA: Tunampenda Magufuli, IGP aandae Polisi kutulinda