Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Juni 9, 2022 ametembelea Kiwanda cha Sukari cha Kagera na kujionea shughuli mbalimbali ikiwemo umwagiliaji, upandaji na uzalishaji wa mbegu bora za kisasa za miwa.

Mbali na kupata maelezo ya uzalishaji huo kutoka kwa Injinia upande wa umwagiliaji mashamba ya miwa Neema Sanaeli, pia Rais Samia amesifiwa kwa utendaji wake wa kazi kwa kulitumikia Taifa , kushughulikia kero za wananchi na kusimamia utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo.

“Mheshimiwa Rais, ili mbegu hizi za miwa ziweze kuleta tija zinahitaji umwagiliaji wa linahitaji umwagiliaji wa maji takribani milimita 1,500 na zaidi kila mwaka na kwa bahati mbaya upande wetu hu wa Kagera Sugar tunapata milimita 800 tu hivyo tuna upungufu,” amesema Eng. Neema.

Amesema Kiwanda hicho pia kimewekeza miundombinu ya Kisasa ya umwagiliaji ambapo kando ya mto Kagera kuna vituo 15 vya umwagiliaji vinavyosambaza maji kwenye mashamba ya miwa vinavyoendeshwa na mitambo ya umeme iliyofungwa ndani ya shamba hilo.

Hata hivyo, Injinia huyo amemuomba Rais kuvilinda Viwanda vya ndani ambavyo vinasaidia kutoa ajira kwa wananchi na kumueleza kuwa uzalishaji bidhaa katika Kiwanda hicho unaongeza pato la mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa Taifa.

Rais, Samia Suluhu Hassan yupo Mkoani Kagera, akikagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika ziara ya siku tatu iliyoanza jana Juni 8, 2022 na ikitarajiwa kukamilika hapo kesho Juni 10, 2022.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 10, 2022
Majaliwa aridhishwa ujenzi wa Ikulu Chamwino