Rais wa Marekani, Joe Biden, amesema ni aibu kwa wabunge kushindwa kumchagua Spika, baada ya mgombea wa chama cha Republican, Kevin McCarthy kwa mara ya tano kushindwa kupata uungwaji mkono wa kura 218 kutoka kwa wabunge wa chama chake, ili kuibuka mshindi.

Biden ameyasema hayo kufuatia hali ya sintofahamu inayoendelea nchini Marekani kwa Wabunge kushindwa kufikia muafaka na kumpata Spika atakayeliongoza Bunge hilo kitu ambacho kinachelewesha taratibu zinazofuata.

Wabunge wanadaiwa kushindwa kufikia muafaka na kumpata Spika atakayeliongoza Bunge hilo. Picha ya The New York Times.

Amesema, “Hali hii inadhalilisha sana nchi yetu na ina maanisha kwamba bunge limeshindwa kabisa kufanya kazi yake na hii ni aibu kubwa sisi ni taifa kubwa duniani.”

Kwa siku ya tatu mfululizo, wamekutana kujaribu kumchagua Spika, wakati huu wabunge 20 wenye msimamo mkali, kutoka chama cha Republican wanaomnyima ushindi mgombea wao, wakitarajiwa kuendeleza na makali yao.

Mikutano ya hadhara: Wananchi wataamua
Maradhi ya nafsi chanzo mmomonyoko wa maadili