Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameahidi kutoa kiasi cha Shilingi milioni moja kwa kila familia za waliofiwa na wale walionusurika kwenye ajali ya MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba 2018.

Fedha hizo ni nje ya zile Sh. 500,000 zilizokabidhiwa kwa wanafamilia waliofiwa ili ziwasaidie katika taratibu za kuhifadhi miili ya marehemu zao.

“Rais ameniagiza kuwa, ataongeza fedha kwa waathirika na atatoa shilingi milioni moja kwa waathirika wote waliopoteza ndugu zao na walionusurika,” amesema Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

Aidha hadi kufikia jana wananchi na wadau mbalimbali walichangia fedha kuunga mkono serikali katika janga kubwa lililoikumba taifa na kupatikana zaidi ya Shilingi milioni 393.

 

Ronaldo, Messi bado tishio, watajwa kikosi bora cha FIFA
Nyota ya Luka Modric yazidi kung'aa

Comments

comments